mpesabusiness
6d ago

Biashara ya uwakala kiukweli kabisa faida ipo nzuri tu kubwa tena bila yakutumia nguvu na akili sana. Ila Kuna vitu muhim Sana vya kuzingatia ili biashara uione ni nzuri na yenye faida kama ndo unaanza jifunze hapa. 1. Cha kwanza cha muhim mtaji. Huwa napenda sana kuwa mkweli ili kuokoa watu wanao taka kuanza biashara hii, mtaji ni kitu kikubwa sana kinafanya mtu apate faida kubwa sana kwenye biashara hii sababu utaweza kuwahudumia wateja karibia wote wanao kuja kwako na biashara hii miamala ndo hela yako wewe Yani watu wanavyo fanya miamala ndo hela wewe unapata. 2. Eneo zuri. Hii ni sehem wewe unafanyia kazi, sio kila eneo eti linafaa kuweka ofisi ya uwakala mengine hayafai kabisa tafuta eneo lenye watu wengi, mzunguko wawatu mfano hospital, mashuleni, chuoni stand, sokoni na mitaa iliyo changamka zaidi hapo utapiga hela niamin Mimi. 3. Kuwa makini sana sana na utapeli. Yani hili ni jambo muhim zaidi zaidi usipokuwa makini apa unaweza pata hasara kubwa ila ukiwa makini nkufatlia mbinu mbali mbali za utapeli itakupunguzia hatari kubwa kutapeliwa. 4. Hap vijana mnao waajili hakikisheni kwanza mnawapa elim ten elim kubwa kuhusu utapeli inavyo fanyika japo sio utajua mbinu zote ila nyingi tushasema hapa ko ukimpa maelekezo kila siku ya utapeli atakuwa makini sana kuliko yeye kuto jua kama hamna utapeli hio ni mbaya sana. Hayo ni mambo muhim. Follow me Mpesa business #MPESA #MixByYas #Airtel #Vodacom
Je wewe ni wakala?
Pakua Wakala Forum ili ujiunge na jukwaa la mawakala wa huduma za kifedha kwenye mijadala mbalimbali.