superagent
Mar 13, 2025
Hakuna picha au video
Post hii haina picha au video ya kuonesha
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA UKIWA WAKALA WA KIFEDHA Hii ni mbaya sana. Matapeli wawili wanaweza shirikiana. Mfano mmoja akawa Tegeta mwingine Pugu, wa Tegeta anaenda Kwa wakala, anazuga anatoa pesa kumbe anayetoa pesa ni wa Pugu. Anatoa unampa Cash anaondoka. Baada ya nusu saa(akishafika mbali kidogo) anarudisha muamala. Huduma kwa wateja wakiTrack umbali wa aliyetoa pesa na wakala alipo wanagundua ni kweli aliyetoa pesa hakuwa kwa wakala. Na hivyo Wanahitimisha kuwa Hajapokea Cash kutoka kwako. Kumbe kiuhalisia aliyepokea Cash ni mwingine na aliyetoa pesa ni mwingine. Wakala unadhulumiwa pesa yako. #MyTake; 1: Mteja anapokuja kuweka pesa usimpe simu yako kujaza namba 2: Unapo hudumia mteja kutoa au kutuma andika muamala kwenye daftari la taarifa za miamala kama kumbukumbu zako 3: Wateja ambao huwa unawahudumia pesa kubwa au wateja ambao hujawahi kuwahudumia (Strangers), ni bora ujifanye hujaona muamala ili akuoneshe sms. Hii inawahusu wanaotoa pesa kwako 4: Tuwe active na messages na simu za huduma kwa wateja. Mteja akiomba reversal utapigiwa simu na usipopokea unaweza kusababisha muamala aliotoa mteja wa mbali akarudisha kirahisi. Kwa maelezo mengine, usikubali kuudumia mteja wa kutoa pesa asiekua katika eneo lako la kazi kwa maana yuko mbali atumiwe code kisha atoe pesa utakuwa umevuka mipaka ya uwakala bora. •Mteja akitoa Pesa kama unahisi ametuma code kwa mtu wa mbali jifanye haujaona sms na uombe uone sms kwake kwa sababu mteja akitoa pesa akiwa mbali akiomba pesa ile kunauwezekano wa pesa kurudi kwa Mteja* 5: Tujitahidi kufuatilia miamala tuyofanya tukipata nafasi pale wateja wanapopungua. Hii iambatane na kukariri wateja(Angalau). 6: Usitoe siri zako za kazi kwa mtu yoyote unae mjua na usie mjua 7: Kua makini na unavyo hesabu pesa usisingizie chuma ulete 8: Mteja anapo kuja kuweka pesa chukua pesa hesabu pesa kisha mhudumie na mteja anapotoa pesa hakiki sms vizuri MAJINA, KIASI na NAMBA YA SIMU. Kamwe usihudumie kabla ya kupokea pesa au kuhakiki sms ya muamala vizuri. 9: Biashara na rafiki/ndugu/jilani weka mbali utaumia 10: Jua kutofautisha hela bandia na halisi au tumia mashine kuhesabia. 11: Kila unapotuma pesa kuwa makini sana yaani hakiki MAJINA, KIASI na NAMBA YA SIMU. Pia kuwa makini mteja asione neno lako la siri. 12. Hakikisha kila Siku unakagua namba zilizoseviwa kwenye simu yako ya wakala*. Usisevu hata namba moja yaani iwe empty. 13. Mpe mteja Code ya wakala usimpe namba ya Wakala* 14. Kama umeajiriwa acha kuwapa simu yako ya mawasiliano wateja kwani matapeli wanaweza ku-Edit wakaweka namba zao kisha wakaacha jina ulilomsevu Boss wako na badae kukutunia ujumbe wa maelekezo utume pesa na ukatuma ukijua ni Boss wako*. 14. Unapo muwekea pesa mteja wa airtel hakiki commission na ukiona 0 cancel maana atakuwa huyo ni wakala mwenzio. Huruhusiwi kumhudumia wakala mwenzio hilo umeingilia jukumu la wakala mkuu japo kwa mara moja haina shida sana kama utakuwa umeamua kumsaidia float. 15. Usipokee maelekezo yanayotolewa na mtu yoyote kwa namba tofauti na namba 100 hata kama atajitambulisha kwa namna yoyote ile. Mwambie apige namba 100 utamsikiliza. 16. Usipokee maelekezo yanayotolewa na mtu yoyote kwa namba tofauti na namba 100 hata kama atajitambulisha kwa namna yoyote ile. Mwambie apige namba 100 utamsikiliza. 17. Usichukue simu ya mteja ili umsaidie kutoa pesa. Ni kosa kisheria kumtolea pesa mteja, mwelekeze atoe mwenyewe, akijifanya anaharaka mwache aondoke. 18. Ukiona muamala umeingia kwenye simu yako hauutambui usikurupuke hata kama utapigiwa simu na mtu amekosea au akajitambulisha ni wakala mkuu, Mwambie apige namba 100 watamrudishia. Usije ukajichanganya ukamtumia, ni kosa kubwa mno kumrudishia hiyo hela maana huruhusiwi kisheria. Ukimtumia tayari umetapeliwa. Rafiki wa kweli wa wakala ni namba 100 19. Mteja wa kuweka pesa hakikiasha unampa karatasi anaandika kwa mikono yake: namba ya simu, kiasi na majina. Usipofanya hivyo, tapeli anaweza kusema amekutajia nyingine na wewe umeweka nyingine na ukijaribu kurudisha muamala utaambiwa umshatolewa maana! Tapeli atakuomba pesa zake au atakuamrisha umwekee maana atasema hujamwekea kumbe kakupa namba nyingiene wapo wawili wanashirkiana kukuibia 20. Usiiamini hela ambayo uliihesabu then mteja akaishika tena kwa namna yoyote ile. Ikirudi kwako ihesabiwe tena usione uvivu au usiiamini. Utapewa hela bandia au makaratasi katikati au utapewa pungufu. Matapeli ni wajanja sana na ni wepesi kufanya namna. 21. Kila siku ukifungua duka lako, kagua ofisi yako vizuri - Till zako, matangazo yako na simu za miamala Kama kuna swali niulize inbox yangu boss #super Agent HITAJI LAKO NDIO KIPAUMBELE CHETU!! Whtspp & Call 0654555758
Je wewe ni wakala?
Pakua Wakala Forum ili ujiunge na jukwaa la mawakala wa huduma za kifedha kwenye mijadala mbalimbali.