mpesabusiness profile

mpesabusiness

6d ago

Post media

Wengi sana mmeniuliza swali hili nikitaka kuwa wakala nafanyaje fanyaje haya twende kazi ausio. Ili uwe wakala hakuna vitu vigum hapana nikawaida tu mambo baazi ya kufata kama haya. 1. Upate lain za uwakala. Hizi ndo lain za kazi yani kiufupi vitendea kazi vikubwa na muhim kwenye uwakala Kuna kutuma pesa Kwa mteja na, mteja kutoa pesa kuja kwako Kwa wakala sasa Kuna lain inabdi uwe nazo ndo uwe wakala zinaitwa till, kazi yake ndo hiyo kutuma pesa na kupokea pesa toka Kwa mteja je unazipataje? Sehem ya uhakika Zaidi nikwenye maduka yao mfano vodashop japo wapo mawakala wanao sajili lain hizo kama Mimi mwenyewe. Vigezo ukienda vodashop au Yasshop. .nida na kitambulisho chake. .tin number . lessen ya biashara Hivyo ndo vitu muhim vya kupata lain za uwakala na pia Kwa wakala so lazima uwe na lessen ya biashara. 2. Mtaji. Kitu kingine cha muhim ni mtaji utao Anza nao sasa baada ya kupata lain hizo ata ukianza na laki tano hawakukatazi ata laki tatu jamaa ni wewe ila atae Anza na laki tano na milion moja sio Kwamba watalingana faida hapana kama wote mnapata wateja basi wa mtaji mkubwa ndo atapata faida kubwa zaidi. 2. Eneo Ukishakuwa na mtaji na lain unatafuta eneo sasa ambalo wewe utalimudu kulipia basi ndo hapo unafanyia kazi kikubwa liwe eneo zuri kila siku nazani nasema Hilo kuhusu eneo zuri mnajua nishawelekeza sana. 3 hii naongeza mwenyewe uwe na elim kidogo ya mpesa. Usifungue mpesa ukawa hujui kabisa kinachoendelea basi lazima utapitia wakati mgum mwanzoni huo ni ukweli usio pingika kabsa kwaiyo tafuta ka elim kidogo jinsi yakujikinga na matapeli na jinsi ya kuzibiti MTAJI wako. Kwaiyo hivyo ndo vitu vinafanya uwe wakala hakuna kingine Mzee wangu na dada yangu na kaka yangu na mdogo wangu. Follow me Mpesa business #MPESA #MixByYas #AirtelKenya #Vodacom

Je wewe ni wakala?

Pakua Wakala Forum ili ujiunge na jukwaa la mawakala wa huduma za kifedha kwenye mijadala mbalimbali.