Kuna wakala kaja kwangu analalamika sana kapoteza hela anaumia sana nikasema umepotezaje eti mteja alikuja na haraka haraka kanitajia namba nirushe nakamuuliza jina limekuja flani mteja akajibu we rusha Mimi na wahi baaada ya kurusha mteja kama dakika tatu pale kasema umeoksea namba sio hio.
Eti mteja akamfosi atume tena na yeye katuma afu kakubali eti hasara.
Ivi nyie mawakala wenzangu mko serious au mnahela za kuchezea ndugu zangu nishatoa sana somo kuwa makini sana na wateja hawa.
1. Anae jifanya anaharaka.
2. Anae jifanya hataki huduma Kwa haraka eti paka watu wote waishe ndo ahudumiwe.
3. Anae taka utume tu hela bila kusema yeye jina linatoka jina gani.
4. Anae penda kuuliza una laki saba kiongozi ndiyo au basi nitumie efu ishirini hao kuwa nao makini sana.
Na wengine tazidi waletea mjue zaidi sasa Kuna vitu mawakala tunasbabisha wenyewe ebu kuwa makini bana.
#MPESA #vodacom