sayalelsabore96gmail
Jun 17, 2026
Hakuna picha au video
Post hii haina picha au video ya kuonesha
Ndugu zangu mawakala habarini za mchana Leo matapeli wamekuja na mbinu mpya. Iko hivi mteja amepigiwa simu na matapeli akaambiwa kuna Tsh 528,000 imeingia kwenye account yako kimakosa hivyo umefungiwa huduma ya kupiga simu hadi urudishe hiyo hela. Jamaa akamwambia hana hela kwenye simu. Tapeli: nenda kwa wakala lakini usimueleze chochote we muulize kama ana hiyo ela mwambie akutumie kwenye simu yako. Mteja: sasa si ili wakala anihudumie inabidi nimpe cash? Tapeli: wewe nenda ukimaliza hela inarudi unatoa tena hapo kwa wakala Mteja: sawa, mteja akaja hadi kwangu. Mteja: vipi kiongozi kwema? Mimi: kwema karibu big Mteja: si unaweka hela? Mimi: ndio, huyu mteja mimi namfahamu vizuri ni mteja wangu, ila leo alitaka kuingia kwenye mtego. Mteja: Akasema kwa sauti ya chini kwa sababu bado alikuwa anaongea nao na aliwarekodi kwa hiyo akaweka simu nyuma akaniambia kwa sauti ya chini kuna mtu amekosea muamala nataka nimrudishie kaniambia nenda kwa wakala akuwekee ili ela irudi. Mimi: nikamuomba kuona meseji ya muamala umefowardiwa, nikamwambia ni matapeli, wakakata simu nikawatext piga wakapiga matapeli nikaongea nao nikamwambia mteja kafika mnasemaje? Tapeli: mpe mteja simu Mimi: nikampa mteja simu nikaongeza loud 🔊 Tapeli: mbona nilikuambia usimueleze wakala chochote? Mteja: sasa nimfiche nini wakati ndio anatakiwa kuweka hela? Mimi: acheni utapeli tafuteni hila mtachomwa moto Tapeli: akakata simu Mteja: wamefunga lain ukipiga inakata tu!? Mimi: nikarestart simu bado ikagoma nikapiga #31# ikafunguka Mteja: asante sana ningeenda kwingine ningeitiwa ata mwizi Mteja ni mwanachuo, kila mtu anaweza kutapeliwa
Je wewe ni wakala?
Pakua Wakala Forum ili ujiunge na jukwaa la mawakala wa huduma za kifedha kwenye mijadala mbalimbali.