Wote mnao taka anza uwakala na mnataka lain kuweni makini sana kama una vigezo vyote Yani leseni, tin number na nida nenda kwenye maduka ya mitandao husika ila kama huna hivyo vitu mtafute wakala ambae unamjua wewe vizuri au muaminifu kwelikweli.
Kuna changamoto imekuja saivi ukitaka lain ya uwakala halotel kuna sheria lazima uweke 100000 ya kianzio ndio lain yako ikipitishwe sasa kuna watu sio mawakala ukishamtumia tarifa hizo za lain yako eti wanatoa hiyo laki moja unakuwa umepigwa nimepokea malalamiko kwa watu wawili kwaiyo ndomaana huwa nasisitiza tafuta wakala ambae unamuani au unamjua ukipuuzia sawa ni wewe.
Na mimi huwa natoa mafunzo kabisa ya maana adi mtu unaanza kazi hakuna kitu hujui ila kwakuwa wa Tanzania tunazarauliana basi ndio hivo wengine wanajikuta kwenye matatizo ambayo wangejifunza isinge wakuta kabisa Yani.
#MixByYas #MPESA #Vodacom