kantisalei profile

kantisalei

Mar 11, 2025

Hakuna picha au video

Post hii haina picha au video ya kuonesha

Baadhi ya Changamoto za wateja: 1. Anakuja anakuta unahudumia mteja mwingine, lakin atataka yeye umhudumie yeye uache aliowakuta😳 2. Mwingine anakuja simu yake touch mbovu au batani hazibonyezeki anakuambia nitolee humo kuna 1,900🤌🏻 na una foleni ya watu, ukimuliza vip mbona simu iko hivi, anakuambia 'toa hiyo lain weka kwenye simu yako"😏 Unajitahid na simu lake bovu unafika mwisho unaambiwa 'salio halitoshi' 🙁unamwabia anakwambia 'kwani kuna bei gani, niangalizie salio'😭 3. Mwingine unafika kwenye jina unamtajia anakwambia "wew hakiki namba tu"🤷🏻‍♂️ 4. Kuna wale anakuja anaongea sauti ya chini au kwa kujiskia, anaomba unamtolea hela kiasi flani, ukishatoa anakuambia sio kiasi hicho mi nilisema nitolee kiasi hiki. 🙌 5. Sasa kuna mwingine utamtajia jina atakubali utatuma hela baadae anakuja anakuambia nimekosea namba namba nisaidie kuizuiaaa☺️ na mda huo una wateja 🤣 6. Kuna wale anakuja anakuta unamsikiliza mtu akitaja namba yake, yeye anachomeka maneno katikati au anakuuliza "kutoa laki makato bei gani?" 🤗 7. Mwingine anakuja anakuambia nitolee hela anakupa simu, hajui kuna sh ngap, simu ina lain mbili na hajui hela ipo mtandao gani 😆 Kiufupi kero zipo nyingi cha muhimu ni uvumilivu na kujua jinsi ya kucheza nazo zisikutoe kwenye mstari, au ukapandisha hasira.

Je wewe ni wakala?

Pakua Wakala Forum ili ujiunge na jukwaa la mawakala wa huduma za kifedha kwenye mijadala mbalimbali.