mathew
Oct 18, 2026
Hakuna picha au video
Post hii haina picha au video ya kuonesha
Habar wadau..! Nina mambo mawili ya kushare nanyi 1. Kuhusu makato yanayowekwa pindi wakala mdogo anapobadilishana flot na wakala mdogo. Ndugu zangu naona jambo hili limeletwa pasipokuzingatia Uhakika wa huduma ya floti kwa mawakala wakuu, nikimaanisha Kuna wakati wakala mkuu huduma zake zinakwisha pindi ambapo wakala wa kawaida(mdogo) anaendelea kuhitaji huduma. Suala hili linakwenda kunugaisha makampuni na kuwabana mawakala hasa wanapohitaji huduma ya float wakati wamekabwa shingoni na penalties. Nashauri makampuni wangetenga muda wa penalties uanzie asubuhi mpaka saa 12 au saa 2 jion kwa sababu kwa muda huo mawakala wengi wakuu wanakua wamefunga. 2. Jambo la pili ni kuhusu miamala ya malipo ya kiserikali kiukweli sijajuaga haya malipo ya serikali yaliletwa kwetu ili tufanye huduma kuisaidia serikali, au yaliletwa tufanye KAZI Kwa kusaidia serikali na wananchi na sisi pia tupate mkate wa kushiba kupitia hiyo miamala. Nasema kwa sababu kamisheni za malipo ya kiserikali kwa kiwango Fulani Cha kifedha hakifanani kabisa na miamala ya huduma nyingine kama ya kuweka/kutoq mpk unajiuliza hivi Mimi nimeajiriwa na serikali au nimejiajiri?? Kuna siku nafanya muamala wa shs 840,000 napata kamishen shs 180 nilichoka kabisa. Hapa nadhani mawakala inabid tuitwe tukae na makampuni ya simu/benk pamoja na serikali waje watueleze haya malipo yaliletwa kwa mlengo upi, kwa sababu mawakala wengi saana wameacha kufanya hii miamala na akifanya ujue ameshabargain na mteja kuhusu ela ya usumbufu. Niwatakie mjadala mwema
Je wewe ni wakala?
Pakua Wakala Forum ili ujiunge na jukwaa la mawakala wa huduma za kifedha kwenye mijadala mbalimbali.