ibraah profile

ibraah

Apr 14, 2025

โ‹ฎ

Hakuna picha au video

Post hii haina picha au video ya kuonesha

Hii ni kwaniaba ya kumstua mteja wako ambae umaenza kuto kumuelewa kwa mfano anakuletea laki 5 au zaidi anakwambia muongezee kiasi frani atakupa badae unamfania hivyo mushy wa siku inaanza kua mazoea sasa ukiona anavuka mipaka mtishe na hicho chuma hapo chini๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡ TAARIFA KWA WATEJA WETU WAHESHIMIWA Tunapenda kuwajulisha kuwa kuanzia sasa, miamala yote ya kifedha inayozidi kiwango cha kawaida au inayohusisha msaada wa fedha (kwa mfano: kuongeza kiasi kwa niaba ya mteja) itakuwa inarekodiwa kwa maandishi rasmi. Hatua hii imelenga: Kuweka uwazi kati ya mteja na huduma zetu. Kuweka kumbukumbu sahihi za miamala. Kuimarisha usalama na uaminifu wa huduma yetu. Tunaomba ushirikiano wenu na tunashukuru kwa kuendelea kutuamini. Asanteni sana.

Je wewe ni wakala?

Pakua Wakala Forum ili ujiunge na jukwaa la mawakala wa huduma za kifedha kwenye mijadala mbalimbali.