lujuo profile

lujuo

Mar 12, 2025

Hakuna picha au video

Post hii haina picha au video ya kuonesha

Habari members.... Nina tukio hapa ningependa kushare.... Jana Kuna mteja alikuja kwenye duka langu mda hua anakuja nilikua na wateja wengi... Nikamsikia akiniuliza wakala vp naweza kuweka 1m Voda?? Nikamjibu ndio. Ilipo fika zam yake ya kuhudumiwa nikamwona ametoa kibunda kikubwa cha elf moja moja!! Nikaaza kuzihesabu zile ela alikua amezipanga vibaya vibaya sana,wakati nahesabu ile ela Kuna wateja wengine wapo pale wanasubiria huduma. Nikakuta zimetimia 1m. nikamwambia nitajie namba,niaandika namba Sasa Kila nikifika sehem ya jina inagoma inasema nihakiki namba ya mteja sio sahihi. Nikamwambia bro hii namba yako itakua na shida. Nikamwona anampigia cm,wakati anampigia cm huyo mtu aliekua anamtumia iyo ela akaniomba na zile ela zake, nikampa akawa amezishikilia mkononi, mimi nikaendelea kuhudumia wateja wengine. Ghafra nikamsikia ananiuliza! Vp unaweza ukawa na float umewekee kwenye tigo?? Nikamjibu ndio. Akanirudishia Tena zile ela. Roho ikanambia nizirudie Tena kuzihesabu, Kumbe amenipa bunda Lingine ambalo amenyofoa nyofoa ela zimepungua jumla zilikua laki 7. Ila amezipanga vzr zinafanana na zile za mwanzo. Tuweni makini.. matapeli wanakuja na njia tofauti tofauti Kila kukicha.

Je wewe ni wakala?

Pakua Wakala Forum ili ujiunge na jukwaa la mawakala wa huduma za kifedha kwenye mijadala mbalimbali.