mpesabusiness
3d ago

Usije Kwa ubish njoo Kwa kujifunza twende pamoja kila hatua uliza Kwa ustarabu sio ubishi wa chuki. Naposema kwamba usinunue bodaboda milion tatu na zaidi weka kwenye uwakala kama kazi hii utafanya mwenyewe apo nieleweke kwanza alafu twende kwenye somo sasa. Biashara ya pikipiki naijua vizuri sana sababu nilianza kuwa bodaboda na ninayo badaboda Kwa sasa hivi pikipiki inaanzia milion tatu sindyo na kila kitu na usajili lazima ifike na laki tatu haya Baada ya kununua ukaanza kazi kumbuka pikipiki inahitaji service atakama ni mpya kama umempa mtu akuandeshee ndo Kuna changamoto nyingi sana mara hesabu Leo tizi mara hiki sababu nyingi sana na Kwa siku pikipiki ni 10000 marejesho maneno mengi ni hivo Kwa siku. Tunakuja kwenye mpesa mtaji wa shilingi Milion tatu ni mkubwa sana na unafaa sana kwenye uwakala na imani na nihivo kama umepata sehem nzuri na unafanya mwenyewe Kwa siku nzima huwezi kosa 20000 nieleewe vizuri kama upo sehem nzuri watu wanafanya Miamala hiyo kulala nayo ni lazima ata zaidi na hiyo ni ya lipa tu bado till mawakala wanajua hili na hamna sijui ufanye service vitu gani sijui Nini hakuna ko unaweza linganisha hivo. Lakini nimesema zingatia haya mtaji huo nilio sema, eneo liwe zuri nishaaelezea sana kuhusu eneo lakufanyia uwakala, huduma iwe nzuri acha zarau, tatu uwe makini sana na watu wanao jifanya matapeli na nirahisi vizuri tu kuepuka hili tena rahisi sana labda utekwe, mtaji wa uwakala usichanganye na mambo yako utunze. Pia biashara ya pikipiki ina presha sana sana kama huna pikipiki za biashara kuelewa hili ni ngum sana Kama ndo umepata hiyo Milion tatu huna nyingine au hujui utaitoa wapi tena bora uendeeshe mwenyewe hiyo pikipiki au utulie zako kwenye uwakala. Kuna watu wanasema uwakala unahitaji umakini sasa Kuna kazi ambayo haitaji umakini basi we kama hauko makini hakuna kazi utaweza. Naomba comment za kuelimisha apo kwenye comment watu wajifunze
Je wewe ni wakala?
Pakua Wakala Forum ili ujiunge na jukwaa la mawakala wa huduma za kifedha kwenye mijadala mbalimbali.