mpesabusiness profile

mpesabusiness

Jun 15, 2026

Post media

Baazi ya mawakala tuache chuki mwisho tutakuwa wachawi sasa yani yani mtu unamuonea tamaa wakala mwenzako kisa anapata watu wengi wewe hupati afu wateja unawaambia eti kwangu hamji mnaenda kule na siku akiwa kafungw msije kwangu, mwehu wewe kabisa. Biashara haiko hivo kabisa yani biashara inatakiwa ujue kwanini kwanza mimi nakosa wateja wanaenda pengine Kuna vitu vingi sana kwenye uwakala vinasababisha Hilo. 1. Kauli mbaya Kwa wateja. 2. Huduma zikiwa hazipatikani yani flot mara hamna, au cash au subiri kwanza nikimbilie flot , hizo zinaweza sababisha kukosa wateja. 3. Kuchelewa sana kufungua ofisi. 4. Kupigwa kitalaam na wazee wa kazi yani usipate wateja kabisa. Hivyo ndo vitu kwanza uchunguze unavyo huna kabla ya kuanza kuweka chuki Kwa wakala mwenzako acha chuki haitokusaidia Chochote kile we jifunze acha ukichwa maji. #MPESASafaricom #MPESA #Vodacom #Airtel #AirtelKenya #MixByYas

Je wewe ni wakala?

Pakua Wakala Forum ili ujiunge na jukwaa la mawakala wa huduma za kifedha kwenye mijadala mbalimbali.