mpesabusiness profile

mpesabusiness

3d ago

Post media

Watu wengi huwa waoga Sana wakiona mtu kaja kufungua ofisi jirani yake hiyo hiyo ya uwakala basi ana nuna nakufikiria atakosa wateja kabisa ila jibu ni ndiyo unaweza wakosa au usiwakose wateja. Mtu akija kufungua karibu yako we muache na usinune ila Kuna vitu vya muhim sana inabidi uvifanye wewe ulie kutwa hapo. 1. Fungua ofisi mapema sana kabla yake. 2. Ukiweza kawia kufunga ofisi kabla yake. 3. Jikinge utavyo weza wewe Kwa imani utayo ona kabisa hii nikutumia tajilinda kuto zurika na mtu sijasema uende Kwa mganga kuchukua dawa ujikinge hpna sijasem hivo Mimi au upige Dua ya maana kweli kweli ofisini kwako sijasema hivo au upige maombi ya ukweli kila siku unapofungua na kufunga sijasema hivo Mimi. 4. Hudumia wateja vizuri Kwa unyenyekuvu mkubwa na Kwa usikivu mkubwa. 5. Tumia mbinu mbadala nunua pakiti la Jojo au pipi mteja akija kufanya muamala mpe jojo mbili au pipi uone show yake kama ataenda pengine. 6. Hakikisha huduma kwako hazikoseni flot na cash na uache kufunga funga ofisi hovyo bila mpangilio. Ukifanya hayo ata waje kumi huto pungukiwa chchote ila usiwe na roho mbaya tu kwamba upate wewe tu kila kitu no. #MPESA #Vodacom #AirtelKenya #MixByYas

Je wewe ni wakala?

Pakua Wakala Forum ili ujiunge na jukwaa la mawakala wa huduma za kifedha kwenye mijadala mbalimbali.