mpesabusiness
Jun 4, 2026

Matapeli Wanakuja Kwa Njia Nyingi Kwenye Huduma za kifedha – Jihadhari!. Biashara ya uwakala imekuwa msaada mkubwa kwa Watanzania wengi, lakini pia imekuwa mlango kwa matapeli kutumia ujanja wao kuiba fedha za watu wasio na tahadhari. Leo hii, utapeli umebadilika sana. Sio tena mtu anakuibia waziwazi – sasa wanatumia akili, lugha nzuri, na mbinu za kukuchanganya. Njia Kuu Wanazotumia Matapeli: 1. Kupiga simu wakijifanya ni wafanyakazi wa kampuni Watakupigia wakisema wanatoka kampuni ya simu, wanakuambia kuna tatizo kwenye akaunti yako au umeshinda zawadi. Mwisho watakuomba PIN – hapo ndo umeshaingia mtegoni. 2. Kutuma SMS za uongo Unaweza kupokea ujumbe unaoonekana halisi kabisa, ukiambiwa umetumiwa pesa kimakosa. Watakuomba urudishe, kumbe hakuna pesa yoyote iliyoingia. 3. Kukuomba uthibitishe miamala Matapeli wanaweza kukwambia kuna muamala umekwama, wanahitaji uthibitisho wako. Wanapokuomba namba ya siri (PIN), ujue huo ni mtego. 4. Kutumia huruma au hofu Wengine watakuambia ndugu yako kapata ajali au kuna dharura, wanataka utume pesa haraka. Wanacheza na hisia zako. 5. Ku-hack line au kutumia namba mpya Wanaweza kutumia namba inayofanana na ya mtu unayemjua au hata kudukua mawasiliano, wakajifanya wao ni mtu wa karibu. Jinsi ya Kujilinda: Kamwe usitoe PIN yako kwa mtu yeyote Hakikisha unathibitisha taarifa kabla ya kutuma pesa Usiamini kila simu au SMS unayopokea Tumia namba rasmi za huduma kwa wateja Kuwa makini hasa unaposhughulika na fedha Hitimisho Matapeli wapo kila mahali na wanazidi kuwa na mbinu mpya kila siku. Ulinzi wako mkubwa ni kuwa makini na kutokukubali kushawishika kirahisi #MPESA #MPESASafaricom #vodacomtanzania #AirtelKenya
Je wewe ni wakala?
Pakua Wakala Forum ili ujiunge na jukwaa la mawakala wa huduma za kifedha kwenye mijadala mbalimbali.