mpesabusiness profile

mpesabusiness

Jun 18, 2026

Post media

MADHARA YA KUMPA MTEJA SIM YA KAZI. ⚠️ Anaweza ku-save namba yako kwa jina la huduma za fedha kama MPESA, Airtel Money au Mixx by Yas, kisha baadaye akatuma SMS za kughushi na kukuonyesha kama amefanya muamala wakati hajafanya. ⚠️ Anaweza kukupigia au kukutumia ujumbe wa kukusumbua nje ya muda wa kazi. ⚠️ Anaweza kujaribu kupata taarifa zako za siri za uwakala kupitia mazungumzo au ujanja mbalimbali. ⚠️ Anaweza kusambaza namba yako kwa matapeli wengine na kuanza kupokea simu nyingi za udanganyifu. ⚠️ Anaweza kutengeneza ushahidi wa uongo kwa kutumia ujumbe aliouhifadhi ili kujaribu kukudanganya au kukuchafua. ⚠️ Anaweza kukutumia viambatanisho au link za utapeli zenye lengo la kuiba taarifa zako. ✅ Ni vizuri mteja asipewe sim ya kazi mkononi. Muonyeshe kiasi alichotuma au ujumbe unaohitajika wewe mwenyewe bila kumpa simu ashike. Usikamilishe muamala mpaka uhakikishe pesa zimeingia kwenye mfumo wako au akaunti husika. #MPESA #Vodacom #mafunzoyauwakala #AirtelKenya

Je wewe ni wakala?

Pakua Wakala Forum ili ujiunge na jukwaa la mawakala wa huduma za kifedha kwenye mijadala mbalimbali.