mhagama
18 June 2026
Hellow,habar za jion wapambanaji wenzangu Nina swali hapa mfano nimemnunulia mteja kifurushi Cha muda wa maongezi voda mbona sizipati zile kamisheni za vocha na muda waaongezi huwa zinalipwa wap
Machapisho yanayoongoza kwa umaarufu
mhagama
18 June 2026
Hellow,habar za jion wapambanaji wenzangu Nina swali hapa mfano nimemnunulia mteja kifurushi Cha muda wa maongezi voda mbona sizipati zile kamisheni za vocha na muda waaongezi huwa zinalipwa wap

mpesabusiness
18 June 2026
Waafrika sisi kitu kinacho changia umasikini nikuto kutaka kujifunza na ujuaji ambao hatujui ivi mtu kujifunza kitu kitanakusaidia mwenyewe bado unaona shida umasikini utatuua kwa hali hii. Jana na leo watu wawili wametapeliwa kwa njia ambayo nishasema sana humu kila siku usimpe mteja hela kama hujazibitisha mumala vizuri na kuzibitisha salio au usimtumie mtu hela bila kukupa hela mkononi kwanza tena leo tu nimetoa somo hilo. Inatakiwa utapeliwe kwa kitu ambacho hatujasema humu asa kila kitu tunasema huku ila hufati we unachukulia kawaida mtu kupigwa milion tatu kizembe hiyo nasema sababu tushasema sana. Miamala mingine mtu ana edit badala ata usome je ni mtandao husika wenyewe jina mpesa au Airtel money yani mtu anakutumia messeg ya kufowadi na wewe unampa hela kabisa Dah. #AirtelKenya #wakala #MPESA #Vodacom #MixByYas

mpesabusiness
18 June 2026
Sasa ndugu zangu ni hivi mteja akija akijifanya chukua sim hii nitolee hela humo laki nne ila nipe laki mbili kwanza nimpe huyu mtu apa ananisumbua chukua ile sim. Afu mwambie hivi chap na kutolea hapa umpe huyo mtu wako wala hakuna shida àpo utangundua vitu viwili. Kama ni kweli utatoa hela yake kwanza utazibitisha salio nkweli umetoa hela imo au laaa utampa hela na sim yake. Kama ni tapeli utajua tu usimpe sim we sema natoa hapa nikupe we si umesema ni kuna hela humu shida iko wapi kama ni tapeli ata ondoka ataacha sim akiacha we wajulishe watu waribu au kama police iko karibu wajulishe hilo àpo unakuwa umepiga kama pele. Unajulisha watu ili akija kusema labda umeiba sim ushahidi uwepo yani asipate chakusema nakama ni tapeli basi harusi ng'ooo Washatuibia sana na sisi tunawapa hasara kidogo. #MPESA #MixByYas #Vodacom #AirtelKenya #crdbbank
smart_brain386
18 June 2026
JAMANI MAWAKALA WENZANGU NAOMBA KUULIZA, MTEJA NIKIMUUZIA LUKU KUPITIA POS, INATAKIWA NIMCHAJI HELA?

mpesabusiness
18 June 2026
USIMRUSHIE MTEJA HELA KAMA BADO HAJAKUPA HELA MKONONI. Kuna baadhi ya matapeli hutuma ujumbe wa uongo au kuonyesha kumbukumbu za malipo zisizo halali ili uwatumie pesa kabla hujapokea fedha. Daima hakikisha umepokea hela mkononi au zimeingia kwenye mfumo rasmi kabla ya kufanya muamala wowote. Kumbuka: Uthibitisho wa kweli ni pesa kupokelewa, si picha ya risiti wala ujumbe wa simu. #MPESA #Vodacom #AirtelKenya #wakala #Uwakala
lucas
18 June 2026
Habar ya asubh mawakala nauliza hivi uki2miwa hela kutoka nje ya nchi kwenye lain ya yas inafikia kwenye akaunt ya mixx by yas

thebosscashpoint
19 June 2026
ASUBUHI NJEMA WAFANYABIASHARA! ☕📈 Watu wengi huamini biashara hukua kwa kuongeza wateja pekee. Lakini ukweli ni huu: 👉 Biashara nyingi hufa si kwa kukosa wateja, bali kwa kukosa takwimu. Ukijua: ✅ Umeingiza kiasi gani leo ✅ Umetoa kiasi gani leo ✅ Faida yako ni kiasi gani ✅ Huduma ipi inalipa zaidi Basi una nafasi kubwa ya kukuza biashara yako kuliko anayefanya kazi kwa makadirio. THEBOSS AGENT SYSTEM imeundwa kusaidia mawakala na wamiliki wa CashPoint kufuatilia biashara zao kwa urahisi, usahihi na kwa wakati halisi. 📌 Rekodi miamala 📌 Angalia faida 📌 Pata ripoti za kila siku 📌 Dhibiti fedha zako kwa ufanisi 💡 Elimu ya Leo: "Kile usichokipima, huwezi kukiboresha." Anza siku yako kwa kufanya maamuzi kwa kutumia data, sio hisia. 📞 Kwa maelezo zaidi kuhusu THEBOSS AGENT SYSTEM: Ackson (THEBOSS) ☎️ 0766717545 #THEBOSSAgentSystem #CashPoint #WakalaSmart #BiasharaYaKidigitali #UsimamiziWaBiashara #FinancialDiscipline #AgentBusiness #DarEsSalaam 🚀🔥

merveille
19 June 2026
Kariri ada za serikali za lipa ya Vodacom itakusaidia wewe wakala

thebosscashpoint
18 June 2026
🚨 JE, UNA BIASHARA YA UWAKALA? 🚨 Bado unaandika hesabu kwenye daftari au kuhesabu kwa kichwa mwisho wa siku? 🤔 THEBOSS AGENT SYSTEM imeundwa kukusaidia kusimamia biashara yako kwa urahisi na usahihi. ✅ Rekodi Cash In & Cash Out ✅ Fuatilia Float kwa wakati halisi ✅ Hesabu Commission kiotomatiki ✅ Ripoti za kila siku na kila mwezi ✅ Fuatilia faida na mwenendo wa biashara ✅ Punguza makosa ya hesabu na upotevu wa fedha 📊 Mfumo huu unafaa kwa: ✔️ M-Pesa ✔️ Airtel Money ✔️ Mixx by Yas ✔️ HaloPesa ✔️ Mawakala wa huduma za kifedha Biashara yako ikikua, lazima na mfumo wako ukue. 🔥 Usisimamie biashara kwa kukisia, simamia kwa takwimu. 📞 WhatsApp: 0766717545 👨💼 Ackson – THEBOSS CASHPOINT 📍 Dar es Salaam #TheBossAgentSystem #WakalaSmart #MpesaAgent #AirtelMoneyAgent #MixxByYas #BiasharaKwaTeknolojia #CashpointManagement

thebosscashpoint
18 June 2026
🚨 JE, UNA BIASHARA YA UWAKALA? 🚨 Bado unaandika hesabu kwenye daftari au kuhesabu kwa kichwa mwisho wa siku? 🤔 THEBOSS AGENT SYSTEM imeundwa kukusaidia kusimamia biashara yako kwa urahisi na usahihi. ✅ Rekodi Cash In & Cash Out ✅ Fuatilia Float kwa wakati halisi ✅ Hesabu Commission kiotomatiki ✅ Ripoti za kila siku na kila mwezi ✅ Fuatilia faida na mwenendo wa biashara ✅ Punguza makosa ya hesabu na upotevu wa fedha 📊 Mfumo huu unafaa kwa: ✔️ M-Pesa ✔️ Airtel Money ✔️ Mixx by Yas ✔️ HaloPesa ✔️ Mawakala wa huduma za kifedha Biashara yako ikikua, lazima na mfumo wako ukue. 🔥 Usisimamie biashara kwa kukisia, simamia kwa takwimu. 📞 WhatsApp: 0766717545 👨💼 Ackson – THEBOSS CASHPOINT 📍 Dar es Salaam

mpesabusiness
17 June 2026
Unaweza kutambua noti bandia za Tanzania kwa kutumia njia rahisi ya "Shika, Tazama na Geuza" ambayo inapendekezwa na Benki Kuu ya Tanzania. � Bank of Tanzania +1 1. Shika (Papasa) Noti halali huwa na sehemu zenye ukwaruzo au hisia maalum unapopapasa. Maandishi na baadhi ya alama huwa zimeinuka kidogo. Noti bandia mara nyingi huhisi kama karatasi ya kawaida. � Bank of Tanzania +1 2. Tazama Kwenye Mwanga Utaona watermark (sura ya Mwalimu Julius Nyerere) ndani ya noti. Utaona tarakimu za thamani ya noti zikikamilika unapoiangalia kwenye mwanga. Kwenye noti bandia, alama hizi mara nyingi hazipo au zinaonekana kama zimechapishwa tu. � Bank of Tanzania +2 3. Geuza Noti Utepe wa usalama (security thread) hubadilisha rangi na kuonyesha mwendo wa mawimbi unapogeuza noti. Kwenye noti za Sh 2,000, Sh 5,000 na Sh 10,000 utaona maandishi kama "BOT 2000", "BOT 5000" au "BOT 10000" kwenye utepe huo ukiweka kwenye mwanga. Pia kuna namba iliyofichika ambayo huonekana vizuri zaidi unapogeuza noti. � Bank of Tanzania +2 Dalili za Haraka za Noti Bandia ❌ Karatasi ni laini sana au ngumu isivyo kawaida. ❌ Rangi zinachuruzika au kufifia kirahisi. ❌ Hakuna watermark ya Nyerere. ❌ Hakuna utepe wa usalama au umechorwa tu. ❌ Namba za serial zinaonekana zisizo za kawaida au zimechapishwa vibaya. � Nukta Habari +1 Ukipata noti unayoihisi ni bandia, usiiingize kwenye mzunguko wa biashara. Wasiliana na kituo cha polisi au ofisi ya karibu ya bot.go.tz� kwa uhakiki zaidi. � Bank of Tanzania +1

mpesabusiness
17 June 2026
VIGEZO VYA KUPATA LINE ZA UWAKALA ✅ NIDA na kitambulisho chake ✅ TIN Number ✅ Leseni ya biashara au leseni inayokubalika kwa usajili wa line za uwakala ✅ Namba za simu ambazo hazijawezeshwa huduma za fedha kama M-Pesa, Airtel Money, HaloPesa n.k. Ukiwa na vigezo hivyo, una nafasi kubwa ya kupata line za uwakala. Kuhusu bei: 🔹 Ukienda moja kwa moja kwenye maduka ya kampuni za simu, mara nyingi gharama huwa ndogo lakini vigezo vinakuwa vingi na mchakato unaweza kuchukua muda. 🔹 Kupitia wakala, gharama inaweza kuwa juu kidogo lakini huduma hupatikana kwa haraka zaidi mradi uwe na vigezo vinavyohitajika. Muhimu: Hakikisha unafuata masharti ya mtandao husika kwani vigezo vinaweza kutofautiana kidogo kutoka kampuni moja kwenda nyingine. Kwa hiyo, chagua njia inayokufaa kulingana na mahitaji yako na haraka unayotaka kupata huduma. 💼📱 #MixByYas #mafunzoyauwakala #Vodacom #NMB #MPESA #AirtelKenya
shadrakapaulo
17 June 2026
Jaman Luku unalipiaje kupitia lain ya uwakalaa na kupata faidaa??
justin
17 June 2026
Jamani naomba kuuliza Leo wamekuja watu wakasema nibonyeze *150*01#ok Chagua 7 ok Chagua 8 ok Chagua 1 wakala mkuu ok Ety kujuwa wakala wangu mkuu hii kitu ipo sahihi au hapna
sayalelsabore96gmail
17 June 2026
Ndugu zangu mawakala habarini za mchana Leo matapeli wamekuja na mbinu mpya. Iko hivi mteja amepigiwa simu na matapeli akaambiwa kuna Tsh 528,000 imeingia kwenye account yako kimakosa hivyo umefungiwa huduma ya kupiga simu hadi urudishe hiyo hela. Jamaa akamwambia hana hela kwenye simu. Tapeli: nenda kwa wakala lakini usimueleze chochote we muulize kama ana hiyo ela mwambie akutumie kwenye simu yako. Mteja: sasa si ili wakala anihudumie inabidi nimpe cash? Tapeli: wewe nenda ukimaliza hela inarudi unatoa tena hapo kwa wakala Mteja: sawa, mteja akaja hadi kwangu. Mteja: vipi kiongozi kwema? Mimi: kwema karibu big Mteja: si unaweka hela? Mimi: ndio, huyu mteja mimi namfahamu vizuri ni mteja wangu, ila leo alitaka kuingia kwenye mtego. Mteja: Akasema kwa sauti ya chini kwa sababu bado alikuwa anaongea nao na aliwarekodi kwa hiyo akaweka simu nyuma akaniambia kwa sauti ya chini kuna mtu amekosea muamala nataka nimrudishie kaniambia nenda kwa wakala akuwekee ili ela irudi. Mimi: nikamuomba kuona meseji ya muamala umefowardiwa, nikamwambia ni matapeli, wakakata simu nikawatext piga wakapiga matapeli nikaongea nao nikamwambia mteja kafika mnasemaje? Tapeli: mpe mteja simu Mimi: nikampa mteja simu nikaongeza loud 🔊 Tapeli: mbona nilikuambia usimueleze wakala chochote? Mteja: sasa nimfiche nini wakati ndio anatakiwa kuweka hela? Mimi: acheni utapeli tafuteni hila mtachomwa moto Tapeli: akakata simu Mteja: wamefunga lain ukipiga inakata tu!? Mimi: nikarestart simu bado ikagoma nikapiga #31# ikafunguka Mteja: asante sana ningeenda kwingine ningeitiwa ata mwizi Mteja ni mwanachuo, kila mtu anaweza kutapeliwa
merveille
18 June 2026
Namna nyingine ya kujinufaisha na faida ya Wakala na mteja wake Tumia hiz mbinu Mkoba Lipa kipochi Utashukuru
sareptabusinessesltd
17 June 2026
Tatizo la float top up Selcom nafikiri ni wakati litatuliwe. Mawakala wakuu wengi hawana.
makenzie42
17 June 2026
Mawakala wenzangu hivi till za super agent Airtel money na halopesa zinavigezo gani kuvipata

merveille
17 June 2026
Hivi ndivyo ofisi yangu ilivyo japokuwa Ai amechangia kwa kiasi kidogo

mpesabusiness
16 June 2026
Ushauri wangu huu kwa wanao taka kuanza uwakala hakikisha lipa yako na till ya voda visiwe vimesajiliwa kwa nida moja hiyo ndo inaleta shida kidogo kwa sasa. Kwaiyo lipa iwe nida ingine na till ya voda iwe nida ingine hiii itakusaidia ila kama unaona nazingua weka zifanane majina. #MixByYas #Vodacom #vodacomtanzania #AirtelKenya #MPESA
Je wewe ni wakala?
Pakua app ili kupenda, kutoa maoni, na kushiriki kwenye mijadala.