sayalelsabore96gmail
4 June 2026
Mfano kwa sasa YAS wana APPLICATION japo bado wanafanya maboresho bado ina vipengele vingi vya maboresho na tuwaombe waweke option za kulipia maji umeme, ada na malipo mengine kama za kibenki ili tuboost COMMISSION
Machapisho yanayoongoza kwa umaarufu
sayalelsabore96gmail
4 June 2026
Mfano kwa sasa YAS wana APPLICATION japo bado wanafanya maboresho bado ina vipengele vingi vya maboresho na tuwaombe waweke option za kulipia maji umeme, ada na malipo mengine kama za kibenki ili tuboost COMMISSION

tonny
4 June 2026
π’ WAKALA, BIASHARA NA WATOA HUDUMA WOTE KARIBUNI π’ Je, unahitaji fomu za muamala zenye muonekano wa kisasa na wa kuvutia kwa biashara yako? Ninatengeneza na kuuza: β Fomu za Kuweka Pesa β Fomu za Kutoa Pesa β Fomu za Kutuma Pesa β Receipt za biashara β Mabango ya matangazo (Posters) β Business Cards β Design mbalimbali za biashara π Muundo wa kisasa na wa kitaalamu π Bei nafuu π Kazi hupatikana kwa haraka π Unawekewa jina la biashara yako na nembo yako Biashara yako ionekane ya kisasa na yenye kuaminika kwa kutumia fomu zenye ubora.

mpesabusiness
4 June 2026
Kuna wakala kaja kwangu analalamika sana kapoteza hela anaumia sana nikasema umepotezaje eti mteja alikuja na haraka haraka kanitajia namba nirushe nakamuuliza jina limekuja flani mteja akajibu we rusha Mimi na wahi baaada ya kurusha mteja kama dakika tatu pale kasema umeoksea namba sio hio. Eti mteja akamfosi atume tena na yeye katuma afu kakubali eti hasara. Ivi nyie mawakala wenzangu mko serious au mnahela za kuchezea ndugu zangu nishatoa sana somo kuwa makini sana na wateja hawa. 1. Anae jifanya anaharaka. 2. Anae jifanya hataki huduma Kwa haraka eti paka watu wote waishe ndo ahudumiwe. 3. Anae taka utume tu hela bila kusema yeye jina linatoka jina gani. 4. Anae penda kuuliza una laki saba kiongozi ndiyo au basi nitumie efu ishirini hao kuwa nao makini sana. Na wengine tazidi waletea mjue zaidi sasa Kuna vitu mawakala tunasbabisha wenyewe ebu kuwa makini bana. #MPESA #vodacom

tonny
4 June 2026
Hii ina ukweli kiasi gani

tonny
4 June 2026
Dah mawakala tuweni makini sana,ningependa ku share kitu hapa mimi alikuja mteja anajifanya ana haraka so na mimi napenda kwenda kasi ili nisimchoshe mteja akanitajia namba ya simu kisha akakosea no Moja Ile pesa ninamuuliza jina anajifanya wewe tuma tu ule nathibitisha ananiambia jina na jina limekuja jingine hela ikapotea akanilazimisha niwekee pesa ingine so nikawa nimepoteza so tuweni makini

mpesabusiness
4 June 2026
Turudi kwenye elim sasa watu wapya waweze kujua taratibu za uwakala ili nao waelewe wasirudie makosa. Kwenye uwakal Kuna Sheria zake kama sehem ingine kwaiyo unapo taka kuanza kazi hii usiishie tu kuuliza faida na hasara ulizia na Sheria zinazo takiwa kwenye kazi hii. Sheria nyingi ambazo watu hawaambiwi. 1.Lipa sio maalum Kwa wakala. Hii ni Sheria japo haijiarishi mnabana wakala au laa ila ni Sheria hasa Vodacom hawataki wakala atumie lipa namba hilo lifaham. 2. Mteja afanye muamala akiwa sehem yako ya kazi. Mitandao haziruhusu mteja atoe hela akiwa mbali na eneo lako la kazi kutokana na usalama wako wa miamala kwenye kurudishwa Kwa muamala. 3. Baadhi ya mtandao kama HALOTEL ndo Sheria kubwa kufanya muamala wakuweka kwenye namba moja Zaidi ya mara mbili. Halotel huwa hawataki urudie urudie kutuma pesa kwenye namba moja ukifanya hivo huwa wanakukata hela 4. Wakala mkuu ndo akuhudumie. Mitandao inasisitiza sana wakala mkuu peke ake ndo akuhudumie wewe wakala ili kuepuka mambo ya utapeli Kwa mawakala. 5. Mteja awe na kitambulisho wakati una muhudumia. Yani mteja aje na kitambulisho cha kura au nida anapokuja kwakoππ Hizo ni baazi ya Sheria muhim sana unazot takiwa kuzijua wewe ambae unataka kuanza uwakala. Follow me Mpesa business Vodacom Halotel Tanzania Yas Tanzania #MPESA #AirtelKenya #vodacom

mpesabusiness
4 June 2026
Hili swala tusaidiane na voda na wenyewe ili turudi huku kwenye till Kwa kufanya hivi Kiuhalisia kurudi haraka tu kwakumwambia mteja kuwa toa Kwa till itakuwa ngum hatutofanya kazi we utagoma mwingine atatumia lipa kutoa ko bado itakuwa ngum Nini kifanyike. Tunaomba voda andae message za kuwapa onyo Kali wateja mfano kuanzia sasa hupaswi kutoa hela kutumia lipa ya wakala tumia till yakawaida sio lipa usipo fanya hivyo lain inafungwa mazima. Hiyo labda ndo itakuwa njia rahisi sana kuturudisha kwenye till tunaomba Vodacom popote malipo mtusikie. Vodacom Tanzania #MPESA #MPESASafaricom #vodacomtanzania

mpesabusiness
4 June 2026
Matapeli Wanakuja Kwa Njia Nyingi Kwenye Huduma za kifedha β Jihadhari!. Biashara ya uwakala imekuwa msaada mkubwa kwa Watanzania wengi, lakini pia imekuwa mlango kwa matapeli kutumia ujanja wao kuiba fedha za watu wasio na tahadhari. Leo hii, utapeli umebadilika sana. Sio tena mtu anakuibia waziwazi β sasa wanatumia akili, lugha nzuri, na mbinu za kukuchanganya. Njia Kuu Wanazotumia Matapeli: 1. Kupiga simu wakijifanya ni wafanyakazi wa kampuni Watakupigia wakisema wanatoka kampuni ya simu, wanakuambia kuna tatizo kwenye akaunti yako au umeshinda zawadi. Mwisho watakuomba PIN β hapo ndo umeshaingia mtegoni. 2. Kutuma SMS za uongo Unaweza kupokea ujumbe unaoonekana halisi kabisa, ukiambiwa umetumiwa pesa kimakosa. Watakuomba urudishe, kumbe hakuna pesa yoyote iliyoingia. 3. Kukuomba uthibitishe miamala Matapeli wanaweza kukwambia kuna muamala umekwama, wanahitaji uthibitisho wako. Wanapokuomba namba ya siri (PIN), ujue huo ni mtego. 4. Kutumia huruma au hofu Wengine watakuambia ndugu yako kapata ajali au kuna dharura, wanataka utume pesa haraka. Wanacheza na hisia zako. 5. Ku-hack line au kutumia namba mpya Wanaweza kutumia namba inayofanana na ya mtu unayemjua au hata kudukua mawasiliano, wakajifanya wao ni mtu wa karibu. Jinsi ya Kujilinda: Kamwe usitoe PIN yako kwa mtu yeyote Hakikisha unathibitisha taarifa kabla ya kutuma pesa Usiamini kila simu au SMS unayopokea Tumia namba rasmi za huduma kwa wateja Kuwa makini hasa unaposhughulika na fedha Hitimisho Matapeli wapo kila mahali na wanazidi kuwa na mbinu mpya kila siku. Ulinzi wako mkubwa ni kuwa makini na kutokukubali kushawishika kirahisi #MPESA #MPESASafaricom #vodacomtanzania #AirtelKenya
lazaromhongole
4 June 2026
Habari za asubuhi mm naona tufungue group la kupeana mawazo kwa mfano kuna Wakala ndo kwanza anaanza hii kazi hawezi kujua Kila kitu kwahyo tukiwa na hilo group anaweza akauliza na mwenye kujua akamjibu ASANTENI SANA
mpesabusiness
4 June 2026
Karibuni mawakala wote humu ndani mpesa business niko huku kuwapa elim yote kuhusu uwakala twende pamoja himiza watu waje huku

mbugi
4 June 2026
Je KAZI ya uwakala inalipa? Namba comment zako hapa chini mdau
emanuelmasele
3 June 2026
Hii kazi ya risk sana asee Yaani mteja anakuja akiondoka hela zinamfata nyuma ! π
nordpay
3 June 2026
Hello Habari Nataka kuanza baishara Ya uwakala Ila Sijui A wala B ila mtaji ninao Nini vya kuzingatiaπ₯Ή
allykhan
3 June 2026
Jamani habari ndugu zangu!! Naomba kujuwa jinsi yakutoa hela mpesa nakuziweka kwenye njia ya till au ya biashara? ALLY KHAN
lazaromhongole
3 June 2026
Habari zenu jama mwenye vitabu vya kujaza miamala tafadhali anisaidie

salome
3 June 2026
Kuhusu mawakala kuacha kutumia lipa Kuna muda Kuna ugum wake tena mkubwa sana. Kwa sasa wateja wengi sana walisha zoea makato ya lipa ndo wanayo taka na hawalalamiki wenyewe Kwao ndo wanaona ni nafuu zaidi sasa Nini labda kifanyike ili mawakala waache kutumia lipa. Labda mitandao iondoe lain za lipa zibaki lain za uwakala na lain za kawaida kama mwanzo apo ndipo kutakuwa na solution. Solution ya pili au njia ya pili lain za uwakala ziwekewe makato kama ya lain za lipa apo ndipo itakuwa nafuu zaidi Kwa mawakala kama mnaruhus wafanya biashara watumie lipa watu wanapo fanya miamala unawakatazaje mawakala wasitumie lipa wakati zote ni biashara? Ukikataza kataza wafanya biashara wote kutumia lipa sababu wote tunalipa Kodi na kila kitu. #Mpesa Business
rodgerz
3 June 2026
Habari ya saa hizi jamani Mimi ni wakala nafanyia kazi wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha nimeanza kazi hii mwaka Jana but laini ya uwakala ya YAS sina nimekua nikihangaika sana document zote nnazo yani licence, Tin na NIDA nilishasajili Pale YAS shop Karatu mara mbili lakini sijafanikiwa kupata Till naombeni msaada ndugu zangu
liz1900
4 June 2026
Guys link ya wale wanaotaka group la kubadilishana mawazo SIO FLOAT!! LINK HII HAPA YA MAWAKALA https://chat.whatsapp.com/HwK5ngspqIA277jWldjWGQ
filoscashpoint
2 June 2026
Ndugu wakala tumebaini kuwa hufanyi huduma ya kutoa pesa kupitia namba yako ya uwakala. Epuka kufungiwa huduma. Tafadhali tumia namba yako kwa miamala ya kutoa. Hiii Ina maana gani
brachofluvugo
2 June 2026
kwann yas wanakata sana Camision kwa sasa
Je wewe ni wakala?
Pakua app ili kupenda, kutoa maoni, na kushiriki kwenye mijadala.